Ungana nasi mwanzoni mwa mwaka kwa ajili ya maombi yanayoambatana na mfungo. Mpendwa, napenda ujue kwamba, tunaitegemea neema ya Mungu kuendesha maisha yetu kwa mwaka mzima. Kwa nguvu zetu sisi wenyewe hatuwezi kufika mahali popote pale. Lakini kwa msaada wa Mungu tunaweza kila jambo kwa Neema yake inayotuwezesha kila siku. Kwa sababu hiyo, ninaomba, tunapoendelea na maombi haya, hebu ungana nasi popote pale ulipo ili tuweze kumuomba Mungu pamoja nawe.
Ufuatao ni muongozo wa maombi mwaka 2014:
- MAOMBI JUU YA FAMILIA:
- Familia hutumiwa na Mungu kama kiota cha kukuzia watu wakuu, kufundishia uadilifu na uaminifu, mahali ambapo watu hujifunza upendo, kumcha na kumtumikia Mungu. Watu hujifunza uongozi, na mengineyo mengi.
- OMBA KUWE NA NDOA IMARA ZINAZOZALISHA FAMILIA MADHUBUTI: Omba watu waolewe na kuoa; Mwa 1:26 - 28; 2:18 - 25; Ebr 13:4; Mith 18:22; Hes 36:6; 1Kor 7:1 - 2. Kemea na kufungaroho mbalimbali zinazozuia watu kuoa na kuolewa, na roho zote zinazochelewesha watu kuoa nakuolewa. Na walio katika ndoa wawe na ndoa zinazoshamiri.
- NDOA ZOTE ZIWE NA UZAZI: Watoto wazaliwe; Mwa 1:28; Kut 23:25 - 27. Kuwe na uzalishaji kiuchumi: Isaya 31:15; Zab 133:3; 127:3 - 5. Omba uzazi kwa wana ndoa, watoto wanaozaliwa wakue. Kusiwe na kuharibu mimba: Kut 23:26; wala utasa; Kut 23:26; Gal 2:20; 2Samw 2:5.
- NDOA ZISIVUNJIKE; ZIWE ZA KUDUMU: Mat 19:3 - 12; 2:14 - 16: Omba watu wawe na mioyo ya unyenyekevu iliyojaa rehema, inayoridhia suruhu. Wawe wanaoshaurika. Kol 3:12 - 20; 2Tim 3:3. Taraka huja kutokana na ugumu wa mioyo: Mat 19:8; Kukosa pendo la kweli: 1Kor 13, na kutokujua uthamani wa ndoa: Ebr 13:4.
- NEEMA NA UPAKO WA KUWA "MUME", "MKE", "BABA", "MAMA". 2Nyak13:2; Efeso 3:14 - 15; Ez 16:44; Omba baba awe baba bora kwa watoto wake, mama awe mama bora kwa watoto wake; mume awe mume bora na wa kweli kwa mke wake; na mke awe mke bora na wa kweli kwa mume wake.
- OMBA NEEMA YA MUNGU KWA WANAWAKE WASIOOLEWA WENYE UMRI MKUBWA: Mungu awe faraja na amani yao; Wapate ulinzi na ushindi; Wamtumikie Mungu kwa furaha; Wanaopenda kuolewa Mungu awape waume wema; Uaminifu kwa Mungu; na Uwezo wa kifedha.
- OMBA KWA AJILI YA WAJANE: Ulinzi, nguvu ya kiuchumi, Wamtumikie Mungu kwa furaha; Faraja ya Kimungu, Wajane vijana wanaopenda kuolewa, waolewe; Uponyaji wa nafsi. 2Falme 4:1 - 7; Isaya 54; Luka 2:36 - 38; Zab 68:5.
- WAGANE: Ulinzi na nguvu ya kiuchumi; Wamtumikie Mungu kwa furaha; Uaminifu kwa Mungu; Uponyaji wa nafsi; Walio ijana wapewa wake.
- YATIMA: Vunja roho ya uyatima; Uhakika + Ufunuo wa kuishi maisha ya mafanikio; na Uponyaji wa nafsi.
- PINGA KWA MAMLAKA YA JINA LA YESU;
- Roho na tabia za kudhalilishana kijinsia (kupigana, kutukanana, n.k)
- Roho ya usagaji, roho ya ushoga
- Utesaji wa watoto
- Roho ya mitala
- Roho ya kuoana ndugu
- Roho ya Yezebeli
- Roho ya Ahabu
- Roho na tabia ya kutelekeza familia
- Roho ya utasa (Wanawake)
- Roho ya ugumba (Wanaime)
- Roho ya uvivu
- Roho ya kutokujali
- Roho ya uasi
- Roho ya kujichua (punyeto)
- Jini mahaba
- Roho ya uasherati + uzinzi
- Roho ya kuacha + kuachika (talaka)
Hii ni sehemu yetu ya kwanza inayobeba maombi kwa ajili yafamilia zetuna mambo yote yahusuyo familia; Mpendwa, naomba uwe na mzigo ndani yako kwa ajili ya familia. Haya si maombi ya kuomba siku moja, ni maombi ambayo unapaswa kuomba siku zote; wakati mwingine kwa kufunga, na wakati mwingine pasipo kufunga. Naamini ukiuelekeza moyo wako kwa Mungu lazima atatenda katika familia yako.
Ni vyema tukaelewa kuwa, NDOA na FAMILIA kwa ujumla wake, tangu mwanzo haikukusudiwa mabaya bali mema. Mungu aliipa utukufu wa juu, hakukuonekana shida wala taabu, au matatizo na uchungu ndani yake; bali ilikuwa ndoa kamilifu, familia kamilifu iliyobeba utukufu wa Mungu. Aidha, Mungu hakumuumba mwanamke tasa wala mwanamume mgumba; aliwaumba wote wakiwa na uzazi, akawabariki akawaambia wazae na kuongezeka. Mungu akumuumba mwanamume pasipo mwanamke, wala mwanamke pasipo mwanamume; Mungu alipomuumbwa mwanadamu, alimuumba mwanamke na mwanamume pamoja; kwa hiyo si mpango kabisa wa Mungu mtu kukosa mwenzi wake.
Kwa sababu hiyo, wewe ambaye umeoa na kuolewa tayari, dai haki na ahadi hii; wewe ambaye bado hujaoa wala kuolewa dai ahadi hii ili hata utakapokuja kuoa au kuolewa uwe tayari umetengeneza mazingira mazuri ya wewe kuingia katika utukufu mkamilifu wa ndoa na familia. Omba kwa ajili ya watoto wako; omba kwa ajili ya mke au mume wako; omba kwa ajili ya wazazi wako. Omba wala usiache; Jua hakika, tunapoomba mambo mabaya huzuiliwa yasitujilie na kutupata, na badala yake mambo mema huachiliwa juu ya maisha yetu; baraka huja na kutupata. Kwa hiyo, basi, Hebu tuombe.
No comments:
Post a Comment