Mama huyu katika picha hii, akiwa mwenye furaha, anashuhudia matendo makuu ambayo Mungu amemtendea siku chache baada ya kujifungua.
Mama huyu alifika katika kanisa la Chemichemi za Uzima akiwa amepitiliza siku za kujifungua kwake. Ilikuwa kama miezi miwili hivi imepeta tangu tarehe ya kujifungua kwake itimie. Kwa maelezo yake alipokuwa amekuja kuhitaji msaada wa maombezi, alisema kuwa madaktari wamethibitisha kuwa siku za kujifungua kwake zimetimia na zimekwishazidi, na ya kuwa yeye mwenyewe hakuwa na dariri ya kujifungua. Ashukuriwe Mungu, mara tu baada ya maombi, siku ya tatu baada ya maombi mama huyu alijifungua mtoto wa kike, tena alijifungua salama. Jna la Bwana libarikiwe.
No comments:
Post a Comment