Chemichemi Za Uzima




MSTARI WA LEO

Muhubiri 7:14
Siku ya kufanikiwa ufurahi,
Na siku ya mabaya ufikiri.
Mungu ameifanya hiyo moja kwenda sambamba na hiyo ya pili,
ili mwanadamu asipate kulijua neno lolote litakalofuata baada yake.



Kwa maombi na maombezi au msaada wowote wa kiroho wasiliana nasi kwa;
Simu Namba: +255 756 066 011; +255 688 891 469; +255 752 184 464; au
Barua pepe: chemichemizauzima11@gmail.com; tulbundala@gmail.com

Bofya hapa kutembelea ukurasa wetu facebook na Ulike

Bofya hapa kututembelea youtube na uangalie video zetu za mafundisho ya Biblia na Ibada zetu

Saturday, 25 January 2014

Mambo ambayo yanazuilia mema yasitujilie na Maombi yetu kutokujibiwa - Sehemu ya Kwanza (A)


Mambo Ambayo Yanazuilia Mema Yasitujilie na Maombi yetu Kutokujibiwa - SEHEMU YA KWANZA

Na Mchungaji Emmanuel N. Manwele


Yapo mambo ambayo yanazuilia mema yasitujilie katika maisha yetu, na hayo mambo husababisha maombi yetu yasijibiwe kabisa. Katika somo hili tutakuwa tunaangalia mambo hayo ili kutupa ufahamu utakaotusaidia kuelewa kwamba, pamoja na kuomba ni namna gani na jinsi gani tutende ili kusababisha maombi yetu kujibiwa na hatimaye mema kutujilia.

Katika sehemu hii ya kwanza tutaangalia mambo mawili yanayosababisha mema yasitujilie au maombi yetu yasijibiwe.

  1. Kanuni ya Kupanda na Kuvuna
  2. Uchungu (unaotokana na wivu, na unaotokana na watu waliokukwaza au kukutendea mabaya)

1. Kanuni ya  Kupanda na Kuvuna. Mwanzo 8:22: "Muda nchi idumupo, majira ya kupanda na kuvuna hayatakoma."
Katika andiko hili, tunaona Mungu akifanya  agano na Nuhu ya kwamba, hataachilia adhabu au hukumu juu ya kundi la watu kwa ajili yakosa la mtu mmoja, Kile anachotenda mtu ndicho yeye mwenyewe atakivuna.

Kama kanunu hii inafanya kazi katika maeneo mengine, ndivyo inavyofanya kazi katika maisha yetu; kama mtu atapanda mabaya, ni lazima atavuna mabaya aliyoyapanda. Asitegemee kuvuna mema wakati mbegu aliyoipanda ni mbaya.

Mabaya unayoyafanya yanaweza kusababisha kanuni ya kupanda na kuvuna ikafanya kazi kinyume na wewe. Badala ya kupata baraka ukajikuta mabaya yanakujilia.

Wagaratia 6:7 - 8;
"Msidanganyike, Mungu hadhiakiwi; kwa kuwa chochcote apandacho mtu, ndicho atakachovuna."

Mpendwa, Kupanda ni kutenda; unapotenda jambo kwa mtu, au kwa kanisa, kwa mtumishi wa Mungu, kwa wapendwa wenzako, kwa taifa lako, au katika huduma fulani, katika kazi, katika biashara, au kwa yoyote yule unakuwa unapanda mbegu; na ulichopanda ndicho utakachovuna. Ukitenda jambo jema, utavuna jambo jema, na ukitenda jambo baya  utavuna jambo baya kwa sababu ndivyo amaandiko yanavyosema. Hii ni kanuni na nisheria katika ulimwengu wa roho inayofanya kazi katika amisha yetu.

Muhubiri 10:8 - 9;
"Mwenye kuchimba shimo, atatumbukia ndani yake, Na yeye abomoaye boma, nyoka atamwuma. Mwenye kuchonga mawe, ataumizwa kwayo, Naye apasuaye miti huona hatari katika hiyo."

Maandiko haya yanaelezea kanuni hii ya  kupanda na kuvuna; kama ukikusudia jambo baya, na ukaanza kupanga namna ya kulitekeleza, na kuanza kulitekeleza, jambo hilo litakuja kwako; kama vile ulivyokuwa umekusudia kwa mwingine na kulitenda, ndivyo litakavyokuja kwako. Kwa sababu hii, kama hutaki mabaya yakujilie, basi, tafuta  kutenda mambo mema kwa watu wote (na hasa jamaa ya waaminio) ili mema yakujilie, la sivyo mabaya yatakujia kwa sababu unapanga mabaya yawapate watu wengine.

Hii inahusika na niliishije jana, niliishije juzi; kwa hiyo inawezekana leo nashindwa kuona mambo mema yakinijilia kwa sababu jana na juzi nilikuwa nakusudia na kutenda mabaya kwa watu wengine. Kwa sababu nilipanda mabaya jane, leo navuna mabaya.

Kwa hiyo, kama tunataka mema yatujie, na maombi yetu yajibiwe, ni muhimu sana tukayachunguza maisha yetu ya nyuma. Kama kuna jambo baya nimewatendea watu, ni muhimu nikaomba rehema kwa Mungu, na kwa watu niliowatendea mabaya kama bado wapo na wanapatikana. Hii ndio njia pekee inayoweza kuzuilia mavuno mabaya yatokanayo na mbegu mbaya niliyoipanda. Iwapo sitafanya hivi, ni lazima mabaya yatanijilia.

Kanuni hii ya Kupanda na Kuvuna ni kanuni inayofanya kazi katika ulimwengu wa roho, haiwezi kugeuzwa na maombi yetu tu, bali ugeuzwa na sisi kugeuka na kuacha kutenda mambo mabaya na kuomba toba na rehema kwa Mungu katika yale mabaya niliyokwisha kuwatendea watu wengine.

Mpendwa, unapoweka malengo yako, na kupanga mipango yako ya mwaka, miaka miwilia au zaidi, ni muhimu sana ukazingatia kanuni hii ya Kupanda na kuvuna, kwa sababu malengo yako yanaweza kuharibiwa na matendo mabaya unayowatendea wengine; pia unaweza kufikia malengo yako iwapo utazingatia kanuni hii kwa kuwatendea watu wengine mema. Malengo mazuri yanaweza kutokufikiwa kwa sababu ya mbegu mbaya unayoipanda; mavuno mabaya yatakuwa kikwazo kwako cha kutoufikia malengo yako mema.

Kama umemuharibia biashara mwenzako leo, kesho na wewe biashara  yako itaharibiwa; Kama ni huduma, au kazi, au familia, au kitu chochote kile ulichoweka mkono wako ili kumuharibia mtu mwingine, kesho na wewe kilicho chako kitaharibiwa. Kama utafanya mabaya kwa mwenzako katika chochote anachofanya, muda utafika na wewe chako kitaharibiwa hata kama utakuwa na malengo mazuri na mipango madhubuti katika hicho unachokifanya. Ni muhimu sana kuzingatia hilo. Malengo mazuri na mipango mizuri bila kufuata kanuni kwa kuwatendea watu mema, hayatatimia kamwe.

Uwezekano wa kutovuna hicho kibaya ulichokipanda upo iwapo utaenda mbele za Mungu kwa kujua, kukubali na kuungama yote uliyoyatenda na kutaka rehema kwa Mungu.
Kwa hiyo, hebu yachunguze maisha yako ya nyuma, angalia kama kuna mabaya uliowatendea wengine; kama yapo, basi, tubu, uombe rehema kwa Mungu. Kama hujui namna ya kuomba, Hebu omba nami maombi haya hapa chini;

"Mungu, Baba yetu uliye mbinguni, Wewe ni Mungu ututakasaye maovu yetu na dhambi zetu; ni Mungu uliyejaa rehema na kweli, Mungu utendaye haki na hukumu pasipokuwa na upendeleo. Sasa naja mbele zako, nimetambua kuwa, kuna mabaya niliyowatendea watu wengine, Baba ninaomba unisamehe, kwa sababu kwa kufanya hivyo, nilipanda pando baya katika maisha yangu litakalonizalia mabaya leo na siku zijazo. Mungu Baba, nisamehe, na uling'oe pando hilo katika maisha yangu, kwa sababu ulisema kuwa, Kila pando usilolipanda wewe utaling'oa; Sasa, Mungu Baba yangu, ng'oa pando hili kwa Jina la Yesu.
Asante Yesu kwa kunisamehe na kung'oa pando hili. Amen.


2.  Uchungu: Uchungu huu upo katika namna mbili;

i) Uchungu unaotokana na wivu; Mpendwa kuwa na wivu kwa ajili ya mafanikio ya mtu mwingine ni jambo baya kabisa. Usimuonee wivu mtu mwingine anayefanikiwa, kwa sababu unapofanya hivyo unajitengenezea sababu ya wewe kutofanikiwa. Laana itakuja juu yako, laana isiyovunjwa na maombi. Laana hii, inavunjwa kwa wewe, kutubu na kugeuka.

Mwanzo 4: 3 - 12:

Tunapoanza kufikiri kwamba mambo yetu hayatunyokei kwa sababu ya watu wengine hapo uchungu huanza kuingia ndani ya mioyo yetu, na hapo tunaanza kuzuilia mema yasitujilie. Wivu hutufanya tufikiri kwamba, mambo mema hayatujilii kwa sababu ya mafanikio ya watu wengine. Lakini, jambo hilo si kweli, kwani ukitenda mema , mema yatakujilia. Ninapoanza kuwa na fikra ya kuwa sifanikiwi kwa sababu ya mtu fulani, wivu huingia ndani yagu, na wivu ni hasira inayomua mtu unayemuonea wivu. Unaweza usichukue kisu au bunduki au silaha nyingine yoyote ili kumuua mtu, lakini pale unapokuwa na wivu dhidi ya mtu mwingine, tayari unakuwa umekwisha muua, kwa sababu, amchukiaye ndugu yake ndani ya moyo wake, tayari amekwisha kumuua. Na kwa sababu hiyo, laana iliyonenwa na Mungu kwa Kaini inaanza kufanya kazi kinyume chako (Mwanzo 4:9 - 12)

Ardhi kwa upande wa wakulima ni ardhi yenyewe, kwa wafanya biashara ni biashara yao, kwa wenye taaruma, ni taaruma yao, kwa wafanya kazi ni kazi zao, kwa wenye huduma ni huduma zao, n.k. Kwa hiyo unapomchukia au kumuonea wivu ndugu yako, unakua umemuua na shughuli yako inalaaniwa, inakua haikuzalii matunda. Itakataa kabisa kukuzalia.

ii)  Uchungu unaokuwanao kwa sababu kuna mtu au watu wamekutendea mabaya: Wapo watu waliokutendea mabaya, na hawa hawatakosa kuwepo, hawatakoma katika dunia. Wapo watu watakukwaza au kukuudhi kwa makusudi au pasipo kukusudia. Lakini kazi inabaki upande wetu sisi tunaoudhiwa, tunaporuhusu uchungu ukae ndani yetu, tunaanza kusababisha nguvu ya uharibifu itufuate na kuanza kufanya kazi katika maisha yetu. Nguvu hii itakuwa inapingana na mema yote yanayotujilia kwa kuachilia mambaya yatupate katika maisha yetu.

Kwa sbabu hiyo, ni muhimu sana tukaepuka kuwa na uchungu mioyoni mwetu, na iwapo itatokea tukawa na uchungu, basi, ni muhimu tukaomba rehema na kuacha au kuondoa uchungu ndani ya mioyo yetu. Mpendwa, kama unauchungu utokanao na wivu, au utokanao na kuudhiwa au kukwazwa, basi, geuka ukaachilie uchungu wako na uombe rehema kwa Mungu, na Mungu atakusamehe. Usipofanya hivyo, usitarajie mema kukujilia, tarajia mabaya kukujilia.



Thursday, 23 January 2014

TAMASHA LA PATAKATIFU PAKE: KUSIFU NA KUABUDU

Kwa wale wakazi wa Morogoro: Usikose katika tamasha la KUSIFU na KUABUDU litakalofanyika tarehe 2/02/2014 kanika kanisa la Canaan Christian Centre Morogoro; Muda ni kuanzia saa 7:00 Mchana mpaka saa 12:00 jioni.  Mada itakayokuwa ikizungumziwa ni "Maana halisi ya Maisha ya Kusifu na Kuabudu" USIKOSE.


Picha Za Matukio ya Semina ya Mtume Maboya Katika Kanisa la Chemichemi za Uzima Dodoma 2013





Picha juu: Mtume Maboya akiwa anafundisha Neno la Mungu

Waumini wakiwa wanamsikiliza Mtume Maboya wakati wa Semina hiyo













Picha Juu, Mtume Maboya akiwa anafanya maombezi kwa wagonjwa mbalimbali waliokuwa wamehudhuria semina hiyo.

Watu wakishangilia na kufurahia matendo na miujiza ambayo Mungu alitenda katika Semina hii


Katika semina hiyo iliyofanyika katika kanisa la Chemichemi za Uzima Area A, Dodoma, Watu waliokuwa wagonjwa wa moyo, na mapafu, waliokuwa na uzito uliopitiliza, waliokuwa wanaumwa meno, figo, na wengine wengi wenye magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na wenye vifafa na upungufu wa akili waliponywa papo kwa papo.


Wednesday, 22 January 2014

Aponywa Jipu Papo kwa Papo katika kitovu chake baada ya kufanyiwa maombi kwa njia ya Simu ya mkononi

Mama Nteze akiwa anashuhudia katika ibada mojawapo ya Jumapili akimshukuru Mungu kwa uponyaji alioupata mara tu baada ya kuombewa kwa njia ya simu.

Mama huyu aliyekuwa na jipu kubwa katika kitovu chake ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda wa miezi saba aliponywa papo kwa papo kwa maombi yaliyofanyika kupitia simu yake ya mkononi. Mama huyu, alikuwa anasikiliza kipindi cha redio kinachokwenda kwa jina la Chemichemi za Uzima, kinachoongozwa na Mchungaji Emmanuel N. Manweli na mke wake Mchungaji Chatherine Manwele wa Kanisa la Chemichemi za Uzima, Calvary Assemblies of God Area A Dodoma. Akiwa anaendelea kusikiliza mafundisho na mahubiri, muda wa maombi uliwadia, ndipo alipoamua kuchukua simu yake na kupiga. Mama huyu alieleza shida yake, kuwa anasumbuliwa na jibu bichi katika kitovu chake kwa muda wa miezi saba (7); Mchungaji alimuambia baada ya kusikiliza shida yake kwamba aweke mkono wake mahali penye jipu na kuuondoa mara tatu; alipoutoa mkono wake mara tatu, alifunua tumbo lake, kumbe! jipu lilikuwa limekauka pale pale.

Haya ndio matendo ya Mungu ya ajabu. Mpendwa, siku chache zijazo tutaanza kukuletea video za shuhuda hizi, ili uone jinsi Mungu aponyavyo na kufungua watu wake.


Tunakushukuru kuwa sehemu yetu!                                                                                                Mungu Akubariki Sana

Kwa maombi na maombezi au msaada wowote wa kiroho wasiliana nasi kwa;
Simu Namba: +255 756 066 011; +255 688 891 469; +255 752 184 464; au
Barua pepe: chemichemizauzima11@gmail.com; tulbundala@gmail.com