Mama Nteze akiwa anashuhudia katika ibada mojawapo ya Jumapili akimshukuru Mungu kwa uponyaji alioupata mara tu baada ya kuombewa kwa njia ya simu.
Mama huyu aliyekuwa na jipu kubwa katika kitovu chake ambalo limekuwa likimsumbua kwa muda wa miezi saba aliponywa papo kwa papo kwa maombi yaliyofanyika kupitia simu yake ya mkononi. Mama huyu, alikuwa anasikiliza kipindi cha redio kinachokwenda kwa jina la Chemichemi za Uzima, kinachoongozwa na Mchungaji Emmanuel N. Manweli na mke wake Mchungaji Chatherine Manwele wa Kanisa la Chemichemi za Uzima, Calvary Assemblies of God Area A Dodoma. Akiwa anaendelea kusikiliza mafundisho na mahubiri, muda wa maombi uliwadia, ndipo alipoamua kuchukua simu yake na kupiga. Mama huyu alieleza shida yake, kuwa anasumbuliwa na jibu bichi katika kitovu chake kwa muda wa miezi saba (7); Mchungaji alimuambia baada ya kusikiliza shida yake kwamba aweke mkono wake mahali penye jipu na kuuondoa mara tatu; alipoutoa mkono wake mara tatu, alifunua tumbo lake, kumbe! jipu lilikuwa limekauka pale pale.
Haya ndio matendo ya Mungu ya ajabu. Mpendwa, siku chache zijazo tutaanza kukuletea video za shuhuda hizi, ili uone jinsi Mungu aponyavyo na kufungua watu wake.

No comments:
Post a Comment